Saturday, February 2, 2013

TAARIFA YA MKUTANO

  Sheikh Ponda Issa Ponda na Swalehe Mukadam wenye kanzu kutoka kushoto
Waislam wote wa Dar es Salaam na maeneo jirani mutangaziwa kukutana kesho inshaallah Juma Pili tarehe 03-Feb-2013 Kwanzia Saa 4 Asubuhi-Mchana. katika Kiwanja cha Nuurul Yaqiin (Uwanja wa Pamba) karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga. Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, kujadili nini cha kufanya kuhusu mateso dhidi ya Masheikh wanaoteseka rumande Shekhe Ponda Issa Ponda na Swalehe Mukadam.

Hatua hiyo, inatokana na Masheikh hao kuendelea kusota rumande baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuweka hati ya kuzuia dhamana dhidi yao.
Sisi kama waislamu tunatakiwa kushikamana katika kamba moja kwa hali na mali, ndugu muislamu upatapo taarifa hii muarifu na mwingine kwani uwepo wako ndio mafanikio ya mkusanyiko huo. Hakuna atakaye tufanyia mambo yetu sisi waislam zaidi ya sisi wenyewe.
Shime alaykum, kujitokeza kwa wingi ili kuonesha mshikamano kaika jambo hili muhimu.
Mwisho
Taarifa hii ni kutokana na: https://www.facebook.com/groups/ahlusunatv/428525543893691/?notif_t=group_activity

No comments: