Wednesday, August 21, 2013

NAFASI ZA KAZI KATIKA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO (TALIRI) NALIENDELE - MTWARA


THE UNITED REPULIC OF TANZANIA
MINISTRY OF LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT

Telegrams: Scientific Mtwara                                   Tanzania Livestock Research Institute
Tel: +255 073 293 4035                                         Naliendele
Fax: +255 073 293 41                                            P. O. Box 509
Email: utafiti@iwayafrica.com                                  MTWARA
            In reply please quote:
            Kumb Na. MLD/NAL/F/2/Vol. 1/38

KWA YEYOTE ANYEHUSIKA:

YAH: NAFASI ZA KAZI KATIKA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO (TALIRI) NALIENDELE-MTWARA

Tafadhali rejeeni kichwa cha habari hapo juu.

Napenda kuwatangazia kuwa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) iliyoanzishwa kwa Sheria Namba 4. Ya mwaka 2012 ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo nafasi za kazi kwa wale watakaopenda kufanya kazi katika Taasisi ua Utafiti wa Mifugo Naliendele-Mtwara. Nafasi zilizopo kwa sasa ni kama ifuatavyo:

Wednesday, August 7, 2013

MAMBO MATATU YANAYOFUATIA RAMADHAN


Zakaatul-Fitwr, 'Iydul-Fitwr Na Swawm Ya Sittatush Shawwaal

Tunakaribia kumaliza mwezi Mtukufu wa Ramadhaan na mambo matatu yafuatayo ya muhimu yanayotukabili yanapasa kuzingatiwa ili tukamilishe Swawm zetu ipasavyo na tupate fadhila zake.

1- ZAKAATUL-FITWR  
Inaitwa Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya Kufuturu au Kufutari) kutokana na kumalizika Swawm ya Ramadhaan. Imefaridhiwa mwaka wa pili wa Hijrah katika mwezi wa Ramadhaan. 
Hikmah Yake
Ni kutwaharisha Swawm ya Muislamu kutokana na maneno machafu, ya upuuzi wakati alipokuwa amefunga kwa kulisha maskini chakula ili nao wapate chakula kizuri siku ya ‘Iyd.

Friday, August 2, 2013

ZAKAATUL FITWR


Zakaah Apewe Nani? 
SWALI
Zakaatul-Fitwr apewe nani? Je, inaruhusiwa kuituma mfano kwa Mujaahidiyn waliko vitani? Au kuitoa katika vyama vinavyokusanya sadaka au kujengea msikiti?

JIBU:
Sifa zote ni za Allaah.
Zakaatul-Fitwr inapaswa kupewa maskini Waislamu katika nchi au mji ambao inatolewa kwa sababu ya usimulizi wa Abu Daawuud kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr ilipwe Ramadhaan kuwalisha watu masikini…."

Inaruhusiwa kuituma kwa masikini wa nchi nyingine ambao watu wake wanahitaji zaidi. Hairuhusiwi kujengea msikiti au kuitoa katika miradi ya sadaka.
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam na utoaji wa Fatwa.