Thursday, April 28, 2016

TABIA NJEMA


Sifa njema zote Anastahiki Allaah Mola wa viumbe wote na rehma na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Jamaa na Swahaba zake wote.
Hivi unajua ndugu yangu Muislam, Allaah Akulinde na Akuhifadhi, kwamba 'amali iliyo bora zaidi na inayopendwa na Allaah Mtukufu na Mtume wake ni tabia njema?
Katika Hadiyth sahihi: Kutoka kwa Sa'ad bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah Anapenda tabia njema na Anachukia tabia mbaya"