Wednesday, April 17, 2013

NGUZO ZA SWALA, VITENDO VYA WAAJIB NA SUNNAH KATIKA SWALA


بسم الله الرحمن الرحيم


Nguzo za Swalah ni 14: Nguzo ni zile ambazo ukiswali na ukaziacha kwa makusudi Swalah yako inabatilika, na ikiwa umeacha kwa kusahau, Swalah yako pia itakuwa haikukamilika hadi urejee kitendo chenyewe au urejee rakaa na kisha mwishoni utoe Sajdatus-Sahw. Lakini ukiwa umesahau nguzo ya Takbiyratul-Ihraam, basi itakubidi uiswali Swalah upya tokea mwanzo.

Saturday, April 13, 2013

WALIOCHOMA MSIKITI TUNDUMA BADO HAWAJAFIKISHWA MAHAKAMANI



Waliochoma msikiti Tunduma bado hawajafikishwa mahakamani. Habari kutoka katika mji huo mdogo katika Mkoa wa Mbeya zinafahamisha kuwa Jeshi la Polisi, linaendelea kuwashikilia watuhumiwa 45 wa vurugu za kuchinja na kuchoma moto Msikiti. Awali Jeshi la Polisi l i l i w a t i a m b a r o n i watuhumiwa wa vurugu na maandamano hayo wapatao 90 na baada ya mahojiano, wamechujwa na kubakia 45. 

Wednesday, April 10, 2013

KUMUANDAA MNYAMA KABLA YA KUCHINJWA - STUNNING




Hii ni njia inayotumika kumuandaa mnyama kabla ya kuchinjwa, nia kuu ya stuning ni kumpunguzia mnyama maumivu wakati wa kuchinjwa, pia huondoa uwezekano wa mnyama kumuumiza mchinjaji na mwisho ni kuongeza ubora wa nyama.

Saturday, April 6, 2013

Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda‘wawakaanga’ Polisi mahakamani

 
 
Gazeti la ANNUUR Na. 1061
RABBIUL THAN 1434,
IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013
Na Bakari Mwakangwale

Watuhumiwa Kesi ya Sheikh Ponda‘wawakaanga’ Polisi mahakamani

Wadai walivamiwa msikitini wakiwa katika ibada.
Waikana BAKWATA na kudai hawazijui kazi zake.
Wasema kiongozi wao ni Qur’an na Sunna za Mtume

MASHAHIDI wa upandewa utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, wamedai askari Polisi waliwavamia na kuwapiga wakiwa katika ibada ya Itiqafu, ndani ya Msikiti wa MarkazChang’ombe, jijini Dar esSalaam, usiku wa Oktoba16, 2012.

Tuesday, April 2, 2013

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013





 Rais Jakaya Mrisho Kikwete


Ndugu Wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi.  Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.