Friday, June 26, 2015

MAKOSA YA WAFUNGAJI



1.   Kutia nia kwa kutamka: Baadhi wanaamini kuwa nia usipoitamka basi haijawa nia. Na pia huwafunza watoto kutamka maneno ya kutia nia, au kuwaamrisha wasikose kwenda kunuizwa msikitini na mashekhe. Itambulike kuwa nia mahali pake ni moyoni na kutamka ni uzushi. 
2.                          Kufunga bila kuswali: Baadhi ya watu wanafunga bila ya kuswali au kutimiza Swalah ipasavyo. Watu kama hawa Swawm zao hazifai kwani Swalah ni nguzo ya Dini ya Kiislamu.