Friday, August 2, 2013

ZAKAATUL FITWR


Zakaah Apewe Nani? 
SWALI
Zakaatul-Fitwr apewe nani? Je, inaruhusiwa kuituma mfano kwa Mujaahidiyn waliko vitani? Au kuitoa katika vyama vinavyokusanya sadaka au kujengea msikiti?

JIBU:
Sifa zote ni za Allaah.
Zakaatul-Fitwr inapaswa kupewa maskini Waislamu katika nchi au mji ambao inatolewa kwa sababu ya usimulizi wa Abu Daawuud kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr ilipwe Ramadhaan kuwalisha watu masikini…."

Inaruhusiwa kuituma kwa masikini wa nchi nyingine ambao watu wake wanahitaji zaidi. Hairuhusiwi kujengea msikiti au kuitoa katika miradi ya sadaka.
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam na utoaji wa Fatwa.
 

Kiasi gani nitoe kwenye zakaatul Fitwr?
SWALI:
assalam aleikum
nilikuwa nataka kujua kiasi gani nitoe kwenye zakkatul fitr,na hizo kilo ni za siku 30? naomba nifafanulia
ahsante

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho 

Kiwango cha Zakaatul-Fitwr ni saa' moja ambayo takriban ni kilo mbili na nusu au tatu ya chakula kinachotumika sana katika mji unaotoa Zakaah. Kwa hiyo ikiwa uko pekee yako basi ni saa' moja. Ikiwa una familia basi kila mmoja umtolee Zakaatul-Fitwr ya kiwango hicho hicho na sio kulipia siku 30.

Mwanafunzi Nchi Za Nje Atoe Zakaatul-Fitwr Au Wazazi Wake Wamtolee?
SWALI:
assalam aleykum warahmatullah wabarakat......
 mi kijana ambaye siichi na wazazi wangu kutokana na usoma malaysia, sasa swali langu ni kuwa tunaamnbiwa tutowe fitri baada ya kumaliza kufunga sasa swali langu ni kuwa inatakiwa mie nitowe hiyo fitri au wazazi wangu wakinitolea inafaa.. naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo.

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 
Ikiwa wazazi wako ndio wenye kukuhudumia wewe kwa kukulipia hayo masomo na matumizi yako yote huko uliko, basi ni wajibu wao kukulipia Zakaatul-Fitwr na watakulipia huko waliko wao.
Lakini kama wewe mwenyewe unacho kipato basi inakupasa ulipe Zakaatul-Ftiwr mwenyewe huko uliko.
Lililo bora zaidi kufanya ni kwamba, ikiwa hali yako ni zaidi ya kujitosheleza huko uliko japokuwa ni wazazi wako ndio wanaokuhudumia na japokuwa wao watakutolea Zakaatul-Fitwr waliko wao, basi ukitowa Zakaatul-Fitwr huko uliko ni kheri zaidi. Hii ni kwa sababu; kwanza sio pesa nyingi za kukulafisha bila shaka kiwango chake ni takriban kilo 2 na nusu au tatu ambayo haitokukalifu pesa nyingi. Pili itakuwa ni kama sadaka yako unayoitoa izidi kukuongezea mema.


Hairuhusiwi Kumpa Zakaatul-Fitwr Mtu Ambaye Umewajibika Kumuhudumia.
  
SWALI
Mimi mwanamke nnayeishi nchi za nje. Nimeolewa nikiwa na watoto saba. Kila mwaka nampelekea mama yangu Zakaatul-Fitwr ambaye anaishi Tanzania, nami ndiye nnayemhudumia kwa mahitajio yake (mwenye mas-uliya naye). Je, naruhusiwa kumpa Zakaah au haifai?

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Maulamaa wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kutuma Zakaah ya fardhi ambayo inajumuuisha Zakaatul-Fitwr kwa mtu ambaye inampasa kumhudumia (kuwa na mas-uliya nao) kama wazazi na watoto.
Inasema katika al-Mudawaanah (1/344):
Je, Vipi kuhusu Zakaah ya mali, kutokana na rai ya Maalik nimpe nani?
Akajibu:
"Usimpe yeyote katika jamaa zako ambaye unapaswa kumhudumia" [mwisho wa kunukuu]
ash-Shaafi'iy kasema katika al-Umm (2/87)
"Asimpe (Zakaah ya mali) baba yake, mama, babu au bibi" [mwisho wa kunukuu]

Ibn Qudaamah kasema katika al-Mughniy (2/509):
“Zakaah yoyote ya fardhi isitolewe kwa wazazi hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani mababu na mabibi) au watoto hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani wajukuu).”

Ibn Mundhir kasema:
"Maulamaa wamekubaliana bila ya kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kuwapa Zakaah wazazi ikiwa hali ya mtoaji ni mwenye kuwahudumia kwa sababu kuwapa Zakaah kutamaanisha kuwa hawahitaji tena awahudumie na manufaa yake yatamrudia yeye. Hivyo ni kama kujipa mwenyewe (hiyo Zakaah) nayo hairuhusiwi. Hali hiyo kadhalika ingelikuwa kama kujilipia deni lake mwenye" [mwisho wa kunukuu]

Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) aliulizwa kuhusu hukmu ya kumpa Zakaatul-Fitwr jamaa ambaye ni masikini:
Akajibu:
"Inaruhusiwa kumpa Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali ya mtu kwa jamaa ambao ni maskini. Bali kuwapa jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo. Lakini sharti kwamba kuwapa sio kwa kuhifadhi mali yake mtu, yaani ikiwa huyo jamaa masikini ni ambaye anapasa kumhudumia. Katika hali hii, hairuhisiwi kumtimizia haja zake kwa kumpa Zakaah kwa sababu akifanya hivyo atakuwa amehifadhi pesa zake mwenyewe kwa kumpa yeye Zakaah na hivyo hairuhusiwi. Lakini ikiwa hana mas-uliya naye ya kumhudumia basi anaweza kumpa Zakaah yake, na kumpa Zakaah yake ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sadaka yenu kwa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo)) [mwisho wa kunukuu] 

Kwa hiyo, hairuhusiwi kwako kuitoa Zakaatul-Fitwr yako kumpa mama yako, bali umhudumie kutokana na mali yako nyingine isiyokuwa ya Zakaah. Na tunamuomba Allaah Akuruzuku rizki kwa wingi"
Na Allaah Anajua zaidi

MtotoWa Kiume Ana Uwezo Mzuri Wa Kifedha Lakini Baba Yake Anashikilia Kumtolea Zakaatul-Fitwr

SWALI:
Baadhi ya Baba wanashikilia kuwatolea Zakaatul-Fitwr watoto wao wakiume ambao wana uwezo mzuri wa kifedha. Afanyeje mtoto?  

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Madamu mtoto anao uwezo, inampasa atoe mwenyewe Zakaatul-Fitwr. Ikiwa Baba atamlipia Zakaatul-Fitwr hakuna ubaya khaswa ikiwa ni mazoea ya Baba kuwatolea watoto wake Zakaatul-Fitwr kila mwaka japokuwa wameshakuwa wakubwa na wafanyakazi. Huenda akapenda kuendelea kufanya hivyo alivyozoea kabla na huenda ikamkasirisha Baba ikiwa mwanawe atamwambia: "Usinilipie Zakaah". Hivyo mtoto ampe fursa Baba yake kumlipia Zakaatul-Fitwr na pia mwenyewe ajitolee. Baadhi ya watu wanachukulia kwamba kuendelea kuwatolea watoto wao Zakaah ni kuendeleza kuambatana na watoto wake na dalili ya kwamba wao bado wako chini ya hifadhi na mas-uliya yake. Hivyo mtoto ampe Baba yake fursa afanye kinachomfurahisha.  
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie tutekeleze yanayopasa kwetu.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid


Zakaatul-Fitwr Ni Chakula, Sio Pesa Na Itolewe Kwa Waislamu Wanaohitaji Pekee

SWALI:
Kitu gani unatoa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr? Ni pesa au mbegu? (chakula). Vipi ikiwa humjui mtu wa kumpa? Je, inaruhusiwa kuitoa katika miskitii au kwa kafiri asiye na mahali pa kuishi au kafiri kwa ujumla? 

JIBU: 
Sifa Zote Ni Za Allaah
Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya kutoa saa' ya tende au saa' ya shayiri (ngano) kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd) [Al-Bukhaariy 1503]
Abu Sa'iydil-Khudriyyi (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr saa' moja ya chakula, au saa' ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au saa' ya tende au saa' ya aqit (mtindi mkavu) au saa' ya zabibu" [Al-Bukhaariy]

Kwa dalili hizo, ni dhahiri kwamba Zakaatul-Fitwr lazima iwe ni chakula, sio pesa. Hivyo lazima tutekeleze ilivyoamrishwa katika Sunnah. Hivyo lipa saa' moja ya chakula chochote kinachotumika na watu katika nchi yako mfano mchele au ngano kwa ajili yako na kila mtu katika nyumba yako. (saa' ni sawa na taqriban Kilo 3). Hairuhusiwi kumpa yeyote isipokuwa Muislamu mwenye kuhitaji. Ikiwa hutopata mtu wa kumpa katika nchi yako, unaweza kumwakilisha mtu mwingine akulipie katika nchi nyingine.

Tunamuomba Allaah Atusaidie pamoja na wewe kutimiza yapasayo Anayoyapenda.
Na Allaah Anajua zaidi.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid

Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr (Sadaka Ya Mwisho wa Ramadhaan)

SWALI:
Baadhi ya miskiti wanaashiria kupokea kiwango cha Zakaatul-Fitwr kutoka kwa watu ili wagawe kwa wanaohitaji kwa ajili yao. Hugawa  bidhaa kama mchele, unga n.k. Je, desturi hii ni sawa?

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Kwa vile imekusudiwa kununua na kugawa bidhaa  kwa wanaohitaji (hizo bidhaa) kwa ajili yao, hivya ni sawa na watapa thawabu Insha Allaah.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid

Wapi Itolewe Zakaatul-Fitwr?
SWALI:
Mimi ni kijana ninayeishi Zanzibar, lakini nimepeleka mtoto wangu wa kike Uingereza kwa ajili ya matibabu na nimefunga Ramadhaan Uingereza. Inanipasa nilipe Zakaatul-Fitwr Uingereza au niwakilishe familia yangu Zanzibar kunilipia? Nini hukmu ya kulipa Zakaatul-Fitwr kwa pesa? Tafadhali tanbihi kwamba Uingereza watu hutoa pesa badala ya chakula.

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Maulamaa (Allaah Awe Radhi Nao) wamesema kwamba Zakaatul-Fitwr inaambatana na idadi ya watu, sio pesa hivyo ilipwe mahali ambapo mtu atakuweko usiku kabla ya 'Iyd.

Ibn Qudaamah amenukuu katika Al-Mughniy [4/134]
"Ama Zakaatul-Fitwr ilipwe katika nchi ambayo yule apasaye kulipa yuko, ikiwa ni mali yake iko hapo au haipo hapo" [mwisho wa kunukuu].
Ama kuhusu kulipa Zakaatul-Fitwr kwa pesa, tumeelezea katika jibu la 'Kiwango Cha Zakatul-Fitwr' kwamba lazima ilipwe katika mfumo wa chakula na kwamba kulipa pesa haikubaliwi.

Hivyo lazima ujitahidi kulipa kwa mfumo wa chakula. Ikiwa masikini atakaata chakula na akataka pesa, basi hakuna ubaya kumpa pesa katika hali hiyo kwa sababu ya kuhitajika zaidi.
Na Allaah Anajua zaidi


Inafaa Kutoa Zakaatul-Fitwr Kwa Familia Ya Mkewe Ambao Wanahitaji?

SWALI:
Inafaa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa familia ya mke wangu ambao wanahitaji?

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Zakaatul-Fitwr itolewe kwa masikini na wanaohitaji kwa sababu Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifaradhisha Zakaatul-Fitwr kuwapa masikini iwe kama ni kutwaharisha Swawm ya mfungaji kutokana na maneno ya upuuzi na machafu" [Imesumiliwa na Abu Daawuud [1609] na ikapewa daraja ya Hasan na An-Nawawiy katika al-Majmuu' [6/126] na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abi Daawuud]

Ikiwa familia ya mke wako ni masikini na wenye kuhitaji, hakuna ubaya kuwapa Zakaatul-Fitwr, bali ni bora zaidi kuliko kuwapa wengine kwa sababu familia ya mke wako (wakwe, mashemeji, mawifi) wana haki kuwahudumia kama ni sehemu ya kumheshimu mke na kumtendea wema na upole. 

Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Allaah Amrehemu) amesema katika an-Nuur 'alaa ad-Darb [682]:
"Hakuna shaka kwamba wakwe, mashemeji na mawifi wana haki ambazo ni zaidi ya mtu mwengine yeyote" [mwisho wa kunukuu]

Tunamuomba Allaah Akujaalie thawabu za sadaka na thawabu za kuwahudumia na kuwatendea wema familia ya mke wako kwa huruma"
Na Allaah Anajua zaidi
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid

Zakaatul-Fitwr Igaiwe Kwa Mtu Mmoja Au Watu Mbali Mbali?

SWALI:
Je, Zakaatul-Fitwr ni kwa ajili ya mtu mmoja pekee au igaiwe kwa wengi?

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa mtu mmoja kwa ajili ya mtu   mmoja na inaruhusiwa pia kuigawa kwa watu zaidi ya mmoja.
Na Allaah ni Mweza wa yote..
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam na utoaji wa Fatwa. Fatwa Namba 1204

Zakaatul-Fitwr Ni Fardhi Kwa Masikini Pamoja Na Familia Yake?

SWALI:
Mtu masikini mwenye majukumu ya familia yake ambayo ni miongoni mwa mama, baba na watoto. 'Iydul-Fitwr inawadia naye ana saa' tu ya chakula. Amlipie nani? 

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Ikiwa hali ya masikini huyu ni kama ilivyoelezewa katika Swali, hivyo alipe saa' ya chakula kwa ajili yake kwani ni ziada ya mahitajio yake na mahitajio ya wale ambao ni wajibu wake kuwahudumia mchana na usiku wa 'Iyd, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Anza kwa nafsi yako kisha kwa wanaokutegemea)) [Imesumulia na Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslimi 2.717, 718, 721, 1034, 1036, 1042]

Kuhusu wanaomtegemea ikiwa hawana chochote cha kujitolea katika Zakaah kwa nafsi zao wenyewe, basi hawakuwajibika kulipa kwa sababu Allaah Anasema:  
 ((Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo)) [2: 286]
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna sadaka isipokuwa kwa yule mwenye njia [mwenye uwezo])) [imesimuliwa na Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslim 2/717 Namba 1034. Naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ninapokuamrisheni kufanya jambo, basi fanyeni kadiri muwezavyo)).

Na Allaah ni Mweza wa yote.. Tunamuomba Allaah Amrehemu Mtume Muhammad na Ahli yake na Maswahaba.
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam na utoaji wa Fatwa


Kuwalipia Makafiri Zakaatul-Fitwr

SWALI:
Watu wengi wana wafanyakazi wa nyumbani (housemaids) wasio Waislamu. Je, walipiwe Zakaatul-Fitwr au inafaa kuwapa chochote katika Zakaatul-Fitwr?

JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Hawalipiwi Zakaatul-Fitwr na haipasi wao kupewa Zakaatul-Fitwr. Ikiwa mtu atawapa baadhi ya Zakaah, haitoshi (kwa maana atakuwa hakutimiza wajibu wa kuilipia). Lakini anaweza kuwatendea wema na kuwapa chochote ambacho hakitokani na Zakaah inayowajibika (kama Zakaatul-Fitwr au Zakaah ya mali inayotimia mwaka).

Na Allaah Anjua zaidi

Wanaishi Nchi Za Ki-Magharibi Na Hawaoni Masikini Wa Kuwapa, Wanaweza Kutuma Zakaatul-Fitwr Nchi Nyingine?

SWALI:
Sisi ni wa-Tanzania tunaoishi Uingereza na hatujui watu masikini wowote hapa. Tumepata mtu wa kuaminika Insha-Allaah, ambaye amesema: "Nipeni pesa nitanunua mchele nusu yake na kugawa kwa masikini, na nusu yake nitawapa pesa". Sababu yake ni kwamba tuko zaidi ya watu 500 hivyo itakuwa shida kwake kununua kiasi kikubwa cha chakula na kukibeba. Pia kwa vile masikini pengine wasitake chochote ila pesa kwa sababu wataweza kuzitumia vizuri zaidi kuliko kupata mchele. Je tumpe pesa au tuwakilishe ndugu zetu huko Tanzania ili watutolee?

JIBU: 
Sifa Zote Ni Za Allaah
Rai ya Maulamaa wengi (wakijumuuisha Maalik, ash-Shaafi'y na Ahmad) ni kwamba hairuhusiwi kutoa pesa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr, bali lazima itolewe kama chakula kama ilivyoamrisha na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Al-Bukhaariy (1504) na Muslim (984) iliyosimuliwa na Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr saa' moja ya tende au saa' moja ya shayiri (ngano) kwa kila mtu, aliye huru au mtumwa, mwanamume au mwanamke, miongoni mwa Waislamu" 
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) aliulizwa:
"Masikini wengi siku hizi wanasema kuwa wanapendekezea kupokea Zakaatul-Fitwr katika mfumo wa pesa badala ya chakula kwa sababu zina manufaa zaidi kwao. Je, inaruhusiwa kutoa pesa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr?

Kwa msaada wa: www.alhidaaya.com

No comments: