Saturday, April 13, 2013

WALIOCHOMA MSIKITI TUNDUMA BADO HAWAJAFIKISHWA MAHAKAMANI



Waliochoma msikiti Tunduma bado hawajafikishwa mahakamani. Habari kutoka katika mji huo mdogo katika Mkoa wa Mbeya zinafahamisha kuwa Jeshi la Polisi, linaendelea kuwashikilia watuhumiwa 45 wa vurugu za kuchinja na kuchoma moto Msikiti. Awali Jeshi la Polisi l i l i w a t i a m b a r o n i watuhumiwa wa vurugu na maandamano hayo wapatao 90 na baada ya mahojiano, wamechujwa na kubakia 45. 

 
 I m e a r i f i w a k u w a watuhumiwa hao, hadi sasa bado wapo rumande huku ikiarifiwa kuwa dhamana
yao imefungwa, mpaka hapo kesi yao itakapo tajwa April 18, 2013. “ Mpaka sasa (jumatano ya wiki hii) bado watuhumiwa h a o h a w a j a f i k i s h w a m a h a k a m a n i , h i v y o h a i j a f a h a m i k a watafunguliwa mashitaka gani, mpaka hapo April 18, inayodaiwa kuwa ndiyo siku watakayopelekwa Mahakamani”. Kilisema chanzo chetu cha habari kutoka Tunduma, kwa njia ya simu. Chanzo hicho kilisema, suala la kuchinja kwa sasa wanachinja Waislamu kama kawaida huku zoezi hilo likisimamiwa na Polisi, ili kuepusha watu wasioruhusiwa kuchinja kujiingiza katika zoezi hilo na kusababisha ghasia nyingine. Hata hivyo Waislamu k a t i k a m j i h u o wamelazimika kufungua
bucha yao maalum chini ya Umoja wa Kiislamu Tunduma, ili kujiridhisha zaidi na uhalali wa nyama na kuepuka na hofu ya kulishwa vibudu. Kwa mujibu wa muumini mmoja wa Kiislamu aliye makazi wa Mji huo, Bw. M w i n s h e h e R a s h i d i , a l i s e m a b u c h a h i y o imepewa jina la  ‘Sisi kwa  Sisi’, iliyopo  katika mtaa wa Majengo, CCM. Bw. Rashid alisema Waislamu wamelazimika kufungua bucha hiyo baada ya sakata la Wakristo kuzidi kushika kasi ya kulazimisha kuchinja, na kupeleka nyama hizo katika mabucha kiholela, kwa kuwa bucha nyingi zinamilikiwa na Wakristo. Naye Ustadhi Abdul- Azizi Madenge, akiongea na Gazeti hili toka Tunduma, alisema kumekuwa na
vikao baina ya viongozi w a d i n i n a S e r i k a l I vimekuwa vikiendelea, ambapo tayari viongozi hao wa Serikali Mkoani Mbeya, wameshafanya vikao vitatu. U s t . M a d e n g e , aliyemhadhiri wa dini ya Kiislamu, aliainisha vikao hivyo vilivyofanyika kuwa ni baina ya Maaskofu na Mkuu wa Wilaya, Masheikh na Mkuu wa Wilaya na cha mwisho kilijumisha makundi yote hayo chini ya Mkuu wa Mkoa. Ust. Madenge, aliyefika katika mji huo kushuhudia kadhia hiyo alisema, Mkuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC) Bw. Othman Diwani pamoja na Afisa Usalama w a Wi l a y a  w a l i f i k a k u s h u h u d i a M s i k i t I ulioathiriwa na Wakristo. Kwa upande wake Amir Kundecha, wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) alisema, Waislamu wanashangaa w a t u h u m i w a h a o kucheleweshwa kufikishwa katika vyombo vya sheria,   ili   hali  suala  lipo  wazi.    A m i r K u n d e c h a ,    alisema moja ya dhulma  w a n a y o i l a l a m i k i a Wa i s l a m u n c h i n i n I sheria kuonekana kali kwa Waislamu na kukosa makali kwa Wakristo, h a t a k a m a m a k o s a yanayofanywa yanawiana   a u y a n a y o f a n y w a n a Wakristo kuwa makubwa zaidi. K i o n g o z i h u y o w a Baraza Kuu, alisema kosa huwa kosa linapofanywa n a M u i s l a m u l a k i n I linapofanywa na Mkristo, huwezi kusikia vishindo, na hunyamaziwa hata linavyomalizwa huwezi kujua mpaka husaulika. A m i r K u n d e c h a alisema, kosa likifanywa na Wakristo, sio tatizo na hufanywa kuwa la mtu na mtu lakini likifanywa na Muislamu litahusishwa na Waislamu na dini yake itahusishwa pia, na hata viongozi wao (Masheikh) kutiwa misukosuko. A m i r i K u n d e c h a alisema, hata vyombo vya habari huwa kimya ikiwa muathirika ni Muislamu, m a t h a l a n i a l i s e m a , Mjini Tunduma Msikiti umechomwa moto, kasha kung’olewa madirisha na milango, lakini hawaandiki Msikiti umechomwa. “Isipokuwa tu, ikitokea katika Kanisa hata kama ufito umeanguka kwa kishido cha Waislamu waliopita nje kwa shughuli zao utaambiwa Waislamu wamevunja Kanisa, na vyombo vya habari vyote vitashupalia ufito huo wa Kanisa.” Alisema.

Chanzo:
Na Bakari Mwakangwale
Gazeti la Annur
ISSN 0856 - 3861 Na. 1066 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA -APRILI 12-18, 2013.

No comments: