JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA
UVUVI
WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA
MIFUGO - LITA
TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA NA ASTASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2015/16
1. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo
ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na
Stashahada kama ifuatavyo:
·
Stashahada
ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma
in Animal Health and Production - DAHP)
·
Astashahada
ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Animal
Health and Production Certificate - CAHP)
·
Astashahada
ya Ufundi Sanifu wa Maabara (Certificate
in Veterinary Laboratory Technology - CVLT)
·
Stashahada
ya Ufundi Sanifu wa Maabara (Diploma in
Veterinary Laboratory Technology
(DVLT)
·
Stashada
ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo (Diploma in Range Management and Tsetse Control)
2. Stashahada Maalum ya
Teknolojia ya Maziwa (Speciliased Diploma
In Dairy Technology) Katika mwaka wa fedha wa 2015/2016, Serikali kupitia
Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake
sita na vituo vyake viwili; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke,
Vituo vya Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi hivyo,
watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi / Vituo vyetu wanachuo wa
ufadhili binafsi watakaopenda kukaa nje ya chuo wanaruhusiwa.
3. Wakala inakaribisha maombi
kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne wanaotaka kujiunga na mafunzo
ngazi ya Astashahada. Pia vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wale wenye
Astashahada katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba kwa ajili ya kujiunga
na mafunzo ngazi ya Stashahada.
4. Kampasi
zitakazohusika na mafunzo hayo ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini:
Na
|
KAMPASI/ KITUO
|
ANUANI
|
KOZI ZITOLEWAZO
|
1.
|
TENGERU
|
S.L.P 3101 Arusha
|
DAHP, SDDT & CAHP (Bweni
na kutwa)
|
2.
|
MPWAPWA
|
S.L.P 51 Mpwapwa
|
DAHP & CAHP(Bweni na
kutwa)
|
3.
|
MOROGORO
|
S.L.P 603 Morogoro
|
DAHP, DRMTC & CAHP
(Bweni na kutwa)
|
4.
|
BUHURI
|
S.L.P 1483 Tanga
|
CAHP(Bweni na kutwa)
|
5.
|
MADABA
|
S.L.P 568 Songea
|
DAHP & CAHP(Bweni na
kutwa)
|
6.
|
TEMEKE
|
S.L.P 39866 DSM
|
CVLT & DVLT (Kutwa)
|
7.
|
MABUKI
|
S.L.P 352 Mwanza
|
CAHP (Bweni na kutwa)
|
8.
|
KIKULULA
|
S.L.P 147 Karagwe
|
CAHP (Bweni)
|
5. Sifa za
mwombaji
i) Stashahada (Diploma – DAHP,
DRMTC, DCVLT) - Miaka miwili (2) kwa wanachuo
waliomaliza kidato cha sita na mwaka mmoja (1) kwa wanachuo waliomaliza cheti
kwa mfumo wa Semesta
Awe amemaliza elimu ya
Kidato cha Sita kufaulu masomo matatu ya Sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia,
Hisabati, Jiografia, Sayansi kimu na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu
kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha subsidiaries mbili kwenye masomo
ya sayansi. AU
·
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal
Health and Production (AHPC), Agrovet
au Certificate in Agriculture and
Livestock Production (CALP) ambayo ni sawa na NTA Level 5 kwenye vyuo
vilivyosajiliwa na NACTE.
ii) Astashahada (Certificate – CAHP, CVLT) – Miaka
miwili (2)
·
Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo matatu ya sayansi
kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, jiografia na Kilimo. Kiwango cha
chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha alama ya D kwenye masomo matatu ya sayansi.
·
iii) Stashahada
Maalum ya Teknolojia ya Maziwa (SDDT) – Miezi sita (6)
·
Mwombaji awe amefaulu katika ngazi ya Stashahada katika fani
zifuatazo: Uzalishaji wa Mifugo (DAP), Afya ya Mifugo (DAH) na Afya na
Uzalishaji wa Mifugo (DAHP).
·
Mwombaji awe amefaulu katika ngazi ya Shahada katika fani zifuatazo:
Sayansi ya Wanyama, Afya ya Mifugo, Teknolojia na Usindikaji wa vyakula
6. Masharti ya
Uombaji
·
Mwombaji atume fomu za maombi ya kozi anayotaka kusomea kwa kujaza fomu akiambatanisha nakala (photocopies) za vyeti vyake vya elimu,
pamoja na cheti cha kuzaliwa.
·
Fomu inapatikana kwenye Kampasi zetu, vituo vyetu vyote na Tuvuti
ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz /organization
/Agencies/LITA
·
Fomu irudishwe na Bank
pay-in slip ya Tshs 20,000/= iliyolipwa kwenye LITA Revenue
Account, NMB Morogoro, Acc. No. 22110003142
·
Fomu zote zitumwe Makao Makuu ya Wakala na siyo kwenye Kampasi za
Mafunzo kwa kutumia anuani ya hapo chini.
7. Gharama za
Mafunzo
Gharama za mafunzo zimeonyeshwa
kwenye fomu ya maombi ambayo inapatikana kwenye Kampasi, vituo vya
Wakala na tovuti ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz /organization
/Agencies/LITA
8. Mwisho wa
kupokea maombi
Mwisho wa kupokea fomu za kujiunga na masomo ni tarehe 15/07/2015.
9. Taarifa kwa
watakaochaguliwa
Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa kwenye magazeti ya Daily
News na Habari Leo, kwenye mbao za matangazo za Wizara, Kampasi, Vituo vyake
vyote na kwenye tovuti: www.mifugouvuvi.go.tz /organization
/Agencies/LITA
10. Utaratibu wa kutuma fomu za maombi
Fomu za maombi zitumwe kwa:
KAIMU MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO - LITA,
Veterinary Complex
131 Nelson Mandela Road
S. L. P 9152,
15487
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment