Friday, May 10, 2013

TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA KILIMO NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

TANGAZO KUHUSU NAFASI ZA MAFUNZO YA KILIMO NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika inatangaza nafasi za mafunzo ya Kilimo ngazi ya Cheti na Diploma kwa mwaka wa masomo 2013/14 kama ifuatavyo:

A.MAFUNZO YA KILIMO NGAZI YA CHETI: MUDA WA MAFUNZO MIAKA 2

CHETI CHA KILIMO (CERTIFICATE IN GENERAL AGRICULTURE)
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  • Mwombaji awe amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu katika kiwango kisichopungua daraja la IV alama 27.
  • Awe na ufaulu katika masomo matatu (3) ya sayansi yafuatayo ; “Physics”, “Chemistry”, “Biology”, “Mathematics”, “Agriculture”  na “Geography”, pamoja na somo laEnglish”.

B.MAFUNZO NGAZI YA DIPLOMA: MUDA WA MAFUNZO MIAKA 2

DIPLOMA YA KILIMO (Diploma in General Agriculture)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo CBG, PCB na CBA. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2).
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

DIPLOMA YA UZALISHAJI WA MAZAO (Diploma in Crop Production)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo CBG, PCB na CBA. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2).
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

DIPLOMA YA UMWAGILIAJI (Diploma in Irrigation)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo PCM, EGM na PGM. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2).
.
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

DIPLOMA YA MATUMIZI BORA YA ARDHI (Diploma in Land Use Planning)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo PCM, PCB, CBG, CBA na PGM. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2)..
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

DIPLOMA YA MATUMIZI YA ZANA KATIKA KILIMO (Diploma in Agromechanization)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo PCM, PGM na EGM. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2).
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

DIPLOMA: MBOGA, MAUA NA MATUNDA. (Diploma in Horticulture)
·         Mwombaji awe amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2010 na 2012 na kufaulu masomo ya sayansi katika moja ya michepuo ifuatayo, PCB, CBG, CBA na CBN. Kiwango cha chini ni alama 17(Principal pass 1, Subsidiary 2).
  • Awe amehitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya NTA level 5 au cheti kutoka katika chuo cha kilimo kinachotambuliwa na serikali.

VIAMBATISHO /MAELEZO MUHIMU
Waombaji wa mafunzo ya kilimo  watume barua za maombi yao kwa njia ya Posta.Barua hiyo iwe na anwani sahihi ya mwombaji pamoja na viambatisho vifuatavyo kulingana na aina ya mafunzo:
  • Nakala ya cheti cha ufaulu Kidato cha IV au cha VI.
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kilimo ngazi ya cheti (NTA Level 5)
  • Barua zilizopitishwa na waajiri(kwa waombaji walioajiriwa).
  • Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kilimo yatatolewa kwenye tovuti ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika:www.kilimo.go.tz
  • Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa Vyuo ambako watakuwa wamepangwa kupitia anwani zao sahihi.
  • Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.kilimo.go.tz  na Vyuo vya Kilimo.

  • Maombi yatumwe kwa wakuu wa vyuo kwa kutumia anwani  zilizoorodheshwa hapo chini:
s/n
Long  term training programmes
Name of Institute
1
·         Diploma in Land Use 
·         Diploma in Irrigation
MATI Igurusi
P.O.Box 336. MBEYA
2
·         Diploma in General Agriculture
·         Certificate in General Agriculture
MATI-Ilonga
P.O.Box 66 KILOSA
3
·         Diploma  Agro mechanization

MATI Mlingano
P.O. Box 5051 TANGA
4
·         Diploma in General Agriculture
·         Certificate in General Agriculture
MATI-Ukiriguru
P.O Box 1434 MWANZA
5
·         Diploma in Crop Production
·         Certificate in General Agriculture
MATI Uyole
P.O. Box 2292 MBEYA
6
·         Diploma in General Agriculture
KATC, MOSHI
P.O. Box 1241 MOSHI
7
·         Diploma in Horticulture
HORTI Tengeru
P.O.BOX 1253, ARUSHA
8
·         Diploma in General Agriculture
·         Certificate in General Agriculture
MATI MTWARA,
P.O Box 121, MTWARA.
9.
·         Diploma in General Agriculture
·         Certificate in General Agriculture
MATI TUMBI,
P.O Box 306, TABORA.
10.
·         Certificate in General Agriculture
ATI MARUKU,
P.O Box 127, BUKOBA.
11.
·         Certificate in General Agriculture
KATRIN IFAKARA,
P.O Box 405, Ifakara,MOROGORO
12.
·         Certificate in General Agriculture
ATI INYALA,
P.O Box 2444, MBEYA.

    MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30.06.2013

    Imetolewa na:
         Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

1 comment:

Unknown said...

Mngekuwa mnatoa namba zenu za simu ndo ingekuwa rahisi