عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ الْعِبَادُ فِيهِ
إلاَّ مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ
مُنْفِقًا خَلَفًا. وَيَقُولُ الأَخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا
تَلَفًا)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah(رضي الله عنه) kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila
siku inayowapambaukia watu kuna Malaika wawili wanateremka, mmoja wao
akiomba: Ee Allaah! Mwenye kutoa [sadaka] mlipe zaidi. Na mwengine
huomba: Ee Allaah! Mwenye kuzuia mpe hasara)).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Inapendekezeka kutoa sadaka kila siku ili kupata du’aa ya Malaika na kukhofu kuombewa hasara.
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾ وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾
5. Basi yule anayetoa, na akawa na taqwa.
6. Na akasadiki Al-Husnaa (tamshi zuri la Tawhiyd – laa ilaaha illa-Allaah).
7. Basi Tunamsahilishia kwa ya sahali.
8. Ama yule afanyaye ubakhili na (anayejidhania kuwa) amejitosheleza.
9. Na akakadhibisha Al-Husnaa (tamshi zuri la Tawhiyd - laa ilaaha illa-Allaah).
10. Basi Tutamsahilishia kwa magumu.
11. Na mali yake haitomfaa, atakapoporomoka (kuangamia Motoni)[2]
- Allaah (سبحانه وتعالى) Ametoa ahadi kumwongezea mwenye kutoa sadaka. [Al-Baqarah 2: 245, 261, Al-Hadiyd 57: 11, Sabaa 34: 39].
- Inafaa kumuombea mtoaji sadaka, Allaah (سبحانه وتعالى) Amlipe zaidi kwa alichotoa, na du’aa kwa bakhili anayezuia kutoa katika Njia ya Allaah (سبحانه وتعالى) hasara panapohitajika.
Credit: alhidaaya.com
No comments:
Post a Comment