عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ
عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ يَحِلُّ لِلْمَرْأَةِ أَنْ تَصُومَ
وَزَوْجُهَا شَاهِدٌ إلاَّ بِإِذْنِهِ. وَلاَ تَأْذَنَ فِي بَيْتِهِ إلاَّ
بِإِذْنِهِ)) متفق عليه وهذا لفظ البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Si
halali kwa mwanamke kufunga Swawm [ya Sunnah] ilhali mumewe yupo
[hakusafiri] ila kwa idhini yake. Wala asimruhusu mtu kuingia nyumbani
kwake ila kwa idhini yake)).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Mwanamke hatakiwi kufunga Swawm ya Sunnah yoyote ila kwanza apate ruhusu ya mumewe, kwani huenda akawa anamhitajia kwa kitendo cha ndoa.
- Mwanamke hapasi kumuingiza mtu yeyote nyumbani kwake bila ya ruhusa ya mumewe.
فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ
Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi (hata) wanapokuwa hawapo (waume zao) kwa Aliyoyahifadhi Allaah[2]
- ‘Ibaadah za Sunnah zinashinda haki ya binaadamu.
- Mke kufuata Shari’ah kama hii itamzuia mume kufanya zinaa.
- Umuhimu wa kuhifadhi haki baina ya mke na mume ((Nao wanawake wanayo haki kwa Shari’ah kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao)).[3]
- Umuhimu wa kujilinda na maasi kwa jinsi ya kwamba hata ‘Ibaadah ya Sunnah kama hii ambayo ni ‘Ibaadah yenye malipo makubwa kutoka kwa Allaahسبحانه وتعالى haitakiwi kutekelezwa. [Hadiyth: ((Kila ‘amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa))].[4]
- Mke kufuata amri ya kutokumuingiza mtu yeyote yule nyumbani kwake. Na kufanya hivyo kutazuia fitna na hatari ya maasi ya zinaa baina yake na wanaume wasio mahaarim wake.
- Utekelezaji wa Uislamu ni nidhamu kamili ya maisha hata katika mas-alah ya nyumba na unyumba. Nidhamu hii ikitofuatwa, basi kunatokea matatizo mengi katika utangamano baina ya mume na mke.
- Kila shari’ah iliyoletwa na Uislamu ina hikma yake kubwa na hivyo Muislamu mwema na mzuri ni yule mwenye kuzifuata bila ya kuwa na uzito au kuchagua baadhi.
Credit: alhidaaya.com
No comments:
Post a Comment