Gazeti la ANNUUR Na. 1061
RABBIUL THAN
1434,
IJUMAA MACHI 8 - 14, 2013
Na Bakari Mwakangwale
Watuhumiwa Kesi ya
Sheikh Ponda‘wawakaanga’ Polisi mahakamani
Wadai walivamiwa msikitini wakiwa katika ibada.
Waikana BAKWATA na kudai hawazijui kazi
zake.
Wasema kiongozi wao ni Qur’an na Sunna za Mtume
MASHAHIDI wa upandewa
utetezi katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, wamedai askari Polisi waliwavamia na kuwapiga wakiwa katika ibada ya Itiqafu, ndani ya Msikiti wa MarkazChang’ombe, jijini Dar esSalaam, usiku wa Oktoba16, 2012.
Mashahidi hao ambao ni washtakiwa katika kesi
hiyo namba 145/2012, walitoa madai
hayo mbele ya HakimMkazi wa Mahakama yaKisutu,
Bi. Victoria Nongwa, walipokuwa wakitoa ushahidi wao mahakamani hapoJumatano wiki hii, na kueleza kuwa wanakana mashtaka yote yanayo wakabili.
Mbali na madai hayo, washtakiwa hao ambao kila mmoja alipanda kizimbani kutoa utetezi wake, kwa ujumla walilikana BAKWATA, wakidai
wanaisikia tu lakini hawaitambui pamoja na Mufti Sheikh Shaaban Simba.Wakiongozwa na Wakiliwao Bw. Juma Nassoro, mashahidi hao walisemakwamba walifika katika Msikitiwa Markaz
Chang’ombe kwa lengo la kufanya ibada ya Itiqafu,
yenye fadhila nyingi miongoni mwa ibada za Kiislamu.
Walidai pamoja na kujiandaa na ibada hiyo, hawakuweza kuitekeleza kwani
ilipofika majira ya saa tisa usiku, muda ambao ndio muafaka kwa ibada hiyo, walisikia vishindo, geti kuvunjwa
na kisha mlango na madirisha ya
Msikiti kuvunjwa na askari kuingia ndani na
viatu vyao na kuanza kuwashambulia. Shahidi
namba moja Bi. Kulthumu Mfaume, ambaye pia ni mshtakiwa namba mbili,
akiwa kizimbani aliiambia Mahakama kuwa alisikia kuna ibada ya
Itiqafu katika Chuo Cha Kiislamu Markazi, ndipo alipolazimika kwenda kwa ajili ya Ibada hiyo. “Usiku tulishtuka baada ya kusikia geti
likivunjwa na mara mlango wa Msikiti nao ulibamizwa
na kuvunjika, kasha niliona askari wakiingia ndan ina mabuti yao, walitupiga sana na walikuwa
wanaume tupu, kisha walituingiza katika magari yao” Alisema Bi. Kulthumu. Bi. Kulthumu alisema pamoja na
kujitetea kwamba wapo katika ibada ya
Itiqafu na kuhoji kosa lao ni nini, alidai askari hao hawakuwaelewa na walizidisha kipigo. Akijibu maswali
ya Wakili
wa Serikali, Bw. Tumaini Kweka, kwamba alipataje taarifa
za ibada hiyo ya Itiqafu, Bi. Kulthumu alisema akiwanjiani
alisikia wakitangaza Msikitini, na kwa kufahamu umuhimu wa ibada hiyo alilazimika kwenda. Alipoulizwa ni nani kiongozi wake, Bi.
Kulthumu alijibu hana kiongozi bali yeye huongozwa na Qur’an na Sunna za Mtume
Muhammad(s .a .w). Kwa upande wake, shahidi namba
mbili Bi. Zainab Mohammed (50),
ambaye katika kesi hiyo ni mstakiwa namba
tatu, akitoa ushahidi wake alisema alikamatwa na askari Polisi akiwa katika Ibadaya Itiqaf ndani ya Msikiti
waChuo Cha Kiislamu Markazi Chang’ombe, na
alipata kipigo kutoka kwa askari hao. Kuhusu
ni wapi alipata taarifa za ibada hiyo, alisema alipata kupitia kwa
muumini mwenzake, ambapo baadaya kufika hapo Markaz, hakufanya shughuli yoyote zaidi ya kufanya
ibada ndani ya Msikiti huo. Alipoulizwa ni
nani mmiliki wa eneo alilokamatiwa, alisema kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, anafahamu kuwa Misikitiyote ni mali ya
Waislamu na kila Muislamu ana haki ya kufanya
ibada yoyote. Shahidi namba tatu Bi.Zaidani
Yusuph (66), aliieleza Mahakama kuwa wakati
alipokuwa ndani ya Msikiti Markaz
Chang’ombe kwa ajili ya ibada ya Itiqaf Oktoba 16 mwaka jana, aliona askari wanaume wakiingia upande wa wanawake usiku
baada yakuvunja geti na mlango wa Msikiti
na kuanza kuwapiga. Shahidi huyo ambaye ni mshatakiwa namba nne, alisema kipigo alichopata kutoka kwa Polisi, alijeruhiwa kidole cha mguuni
huku askari hao wakitoa maneno yakejeli.
“Kwa umri wangu huu sikufanya ubishi wowote, lakini walinipiga licha
ya kuwauliza kosa langu ni nini, walizidisha kipigo na walifanya
unyama mkubwa.”Alisema Bibi huyo.Wakili wa
Serikali Bw.Tumaini Kweka, alipomuuliza
ni nani kiongozi wake akiwakama Muislamu, Bi. Zaidan alijibu kwa kujiamini kuwa kiongozi wake ni
Qur’ an na Sunna na hata alipoulizwa nani
msimamizi wake alisema hana zaidi ya Qur’ an. Wakili
Kweka alipomuuliza kama anaifahamu
BAKWATA, Bi. Zaidani, alisema, “Siijui, sitaki kuijua wala sitakikuisikia,
hata huyo Mufti, simjui.” Akitoa
ushahidi wake mbele ya Hakim Bi. Victoria Nongwa, shahidi namba
tano, Juma (22), alisema ilimlazimu kuacha
ibada zake majira ya saa tisa usiku mara baada ya kusikia vishindo nje, kwani geti
lilivunjwa ukafuatia mlango wa
msikiti na kasha aliona askari Polisi wakiingia ndani ya msikiti. Alisema mara baada yakuingia msikitini walianza kuwapiga na kuamuru wafanye wanavyotaka wao. Aliongeza kuwa Walivamia bila kutoa
tangazo lolote na kwamba, vurugu zao ndizo zilizokuwa
ishara kuwa eneo hilo kwa muda huo halikuwa shwari.” Alisema Juma. Naye
alipoulizwa kama anaifahamu BAKWATA, alisema anaifahamu kuwa ni Taasisi ya
Kiislamu kama zilivyo taasisi zingine za dini. Baada ya kuulizwa kama ana mahusiano
na chombo hicho alijibu kuwa haimuhusu. “Tukiwa ndani ya msikiti majira ya saa nane usiku kwenda tisa, tulisikia kishindo nje, kabla hatujakaa sawa tulisikia mlango wa msikiti ukibamizwa na mara waliingia askari kama
wale (akionyesha baadhi ya askari FFUwaliokuwa
mahakamanihapo) na waliingia na viatu vyao Msikitini.” Alisema shahidi huyo namba tano, Bi. Farida Lukoko
(53). Bi. Farida ambaye ni mshitakiwa namba 7, alionyesha Mahakamani
hapo alama za majeraha mikononi mwake,
alisema kuwa alipigwa marugu mikononi
na mgongoni, jambo ambalo alidai kuwa
hadi sasa bado anasikia maumivu
makali katika sehemu hizo. Alisema kipigo
hicho kilimfanya asijitambue baadaya kuanguka chini. Baadaye alielezwa na wenzake kuwa alinyanyuliwa na
askari haokwa kushikwa miguu na mikono
kisha kurushwa ndani ya gari. Shahidi mwingine ambaye ni mshitakiwa namba tisa Athumani Salim, alipoulizwa kama anaifaham Bakwata, alisema anaisikia tu, lakini inajishughulisha na nini, hajui. Alipoulizwa
ni wapi anapta taarifa za kuandama kwa mwezi, alisema Waislamu wanafunga na
kufungua kwa mujibu wa Qur’an na Sunna, popote unapoandama au kwa kukamilika
kwa idadi ya siku katika mwezi huo. Naye shahidi namba nane Adama Ramadhani (40), aliulizwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Bw. Kweka, kama anafahamu kazi za Bakwata, alisema anachojua kazi yakekubwa ni kuwatangaziaWaislamu
mwezi wa Ramadhani unapoandama na
pindi unapomalizika na sivinginevyo. Kwa
ujumla Mashahidi wote walidai
Mahakamani hapo kuwa, hakuna shahidi yeyote upande wa mashtaka aliyewataja kuwa ni wavamizi wa kiwanja wanachoshutumiwa kuvamia. Washtakiwa hao wameanza kutoa utetezi wao Jumatano wiki hii kufuatia Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Bi. Victoria
Nongwa, Jumatatu wiki hii kusema Sheikh
Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wana kesi
yakujibu.Washitakiwa wote wanakabiliwa na makosa manne, isipokuwa
mshtakiwa namba moja (Sheikh Ponda) na
mshtakiwa namba tano (Ust. Mukadam),
ambao wanakabiliwa na mashtaka matano.
Hakimu Nongwa alisema pamoja na
Mawakili wa upande wa utetezi kutoa maelezo ya kina katika utetezi wao juu ya
shauri hilo, Mahakama imeona ni vyema iwape
nafasi washitakiwa waweze kupanda
kizimbani kutoa utetezi wao. “Mahakama
inaona washtakiwa wote waliokamatwa katika kiwanja kile, ni vyema wapande kizimbani ili watoe utetezi wao,
waseme sababu zilizofanya waingie pale.”Alisema
Hakimu Nongwa. Kwa mujibu wa Wakili wa upande wa utetezi Bw. Juma Nassoro,
ameieleza mahakama hiyo kuwa jumla ya
mashahidi sitini watafika mahakani hapo kutoa
ushahidi wao upande kwa upande wa utetezi.
No comments:
Post a Comment