Zakaah Apewe Nani?
SWALI
Zakaatul-Fitwr apewe nani? Je,
inaruhusiwa kuituma mfano kwa Mujaahidiyn waliko vitani? Au kuitoa katika vyama
vinavyokusanya sadaka au kujengea msikiti?
JIBU:
Sifa zote ni za Allaah.
Zakaatul-Fitwr inapaswa kupewa
maskini Waislamu katika nchi au mji ambao inatolewa kwa sababu ya usimulizi wa
Abu Daawuud kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu
'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr ilipwe Ramadhaan kuwalisha watu
masikini…."
Inaruhusiwa kuituma kwa masikini wa
nchi nyingine ambao watu wake wanahitaji zaidi. Hairuhusiwi kujengea msikiti au
kuitoa katika miradi ya sadaka.
Halmashauri
ya Kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam na utoaji wa Fatwa.
Kiasi
gani nitoe kwenye zakaatul Fitwr?
SWALI:
assalam aleikum
nilikuwa nataka kujua kiasi gani
nitoe kwenye zakkatul fitr,na hizo kilo ni za siku 30? naomba nifafanulia
ahsante
JIBU:
Sifa zote njema
Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu
zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka
Siku ya Mwisho
Kiwango cha Zakaatul-Fitwr ni saa'
moja ambayo takriban ni kilo mbili na nusu au tatu ya chakula kinachotumika
sana katika mji unaotoa Zakaah. Kwa hiyo ikiwa uko pekee yako basi ni saa'
moja. Ikiwa una familia basi kila mmoja umtolee Zakaatul-Fitwr ya kiwango hicho
hicho na sio kulipia siku 30.
Mwanafunzi Nchi
Za Nje Atoe Zakaatul-Fitwr Au Wazazi Wake Wamtolee?
SWALI:
assalam
aleykum warahmatullah wabarakat......
mi
kijana ambaye siichi na wazazi wangu kutokana na usoma malaysia, sasa swali
langu ni kuwa tunaamnbiwa tutowe fitri baada ya kumaliza kufunga sasa swali
langu ni kuwa inatakiwa mie nitowe hiyo fitri au wazazi wangu wakinitolea
inafaa.. naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu
wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na
watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ikiwa
wazazi wako ndio wenye kukuhudumia wewe kwa kukulipia hayo masomo na matumizi
yako yote huko uliko, basi ni wajibu wao kukulipia Zakaatul-Fitwr na
watakulipia huko waliko wao.
Lakini
kama wewe mwenyewe unacho kipato basi inakupasa ulipe Zakaatul-Ftiwr mwenyewe
huko uliko.
Lililo
bora zaidi kufanya ni kwamba, ikiwa hali yako ni zaidi ya kujitosheleza huko
uliko japokuwa ni wazazi wako ndio wanaokuhudumia na japokuwa wao watakutolea
Zakaatul-Fitwr waliko wao, basi ukitowa Zakaatul-Fitwr huko uliko ni kheri
zaidi. Hii ni kwa sababu; kwanza sio pesa nyingi za kukulafisha bila shaka
kiwango chake ni takriban kilo 2 na nusu au tatu ambayo haitokukalifu pesa
nyingi. Pili itakuwa ni kama sadaka yako unayoitoa izidi kukuongezea mema.
Hairuhusiwi Kumpa
Zakaatul-Fitwr Mtu Ambaye Umewajibika Kumuhudumia.
SWALI
Mimi mwanamke nnayeishi nchi za nje.
Nimeolewa nikiwa na watoto saba. Kila mwaka nampelekea mama yangu
Zakaatul-Fitwr ambaye anaishi Tanzania, nami ndiye nnayemhudumia kwa mahitajio
yake (mwenye mas-uliya naye). Je, naruhusiwa kumpa Zakaah au haifai?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Maulamaa wamekubaliana bila ya
kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kutuma Zakaah ya fardhi ambayo inajumuuisha
Zakaatul-Fitwr kwa mtu ambaye inampasa kumhudumia (kuwa na mas-uliya nao) kama
wazazi na watoto.
Inasema katika al-Mudawaanah
(1/344):
Je, Vipi kuhusu Zakaah ya mali,
kutokana na rai ya Maalik nimpe nani?
Akajibu:
"Usimpe yeyote katika jamaa
zako ambaye unapaswa kumhudumia" [mwisho wa kunukuu]
ash-Shaafi'iy kasema katika al-Umm
(2/87)
"Asimpe (Zakaah ya mali) baba
yake, mama, babu au bibi" [mwisho wa kunukuu]
Ibn Qudaamah kasema katika al-Mughniy
(2/509):
“Zakaah yoyote ya fardhi isitolewe
kwa wazazi hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani mababu na mabibi) au
watoto hata mstari (wa ukoo) ukifikia vipi (yaani wajukuu).”
Ibn Mundhir kasema:
"Maulamaa wamekubaliana bila ya
kukhitilafiana kwamba hairuhusiwi kuwapa Zakaah wazazi ikiwa hali ya mtoaji ni
mwenye kuwahudumia kwa sababu kuwapa Zakaah kutamaanisha kuwa hawahitaji tena
awahudumie na manufaa yake yatamrudia yeye. Hivyo ni kama kujipa mwenyewe (hiyo
Zakaah) nayo hairuhusiwi. Hali hiyo kadhalika ingelikuwa kama kujilipia deni
lake mwenye" [mwisho wa kunukuu]
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn
(Rahimahu-Allaah) aliulizwa kuhusu hukmu ya kumpa Zakaatul-Fitwr jamaa
ambaye ni masikini:
Akajibu:
"Inaruhusiwa kumpa
Zakaatul-Fitwr na Zakaah ya mali ya mtu kwa jamaa ambao ni maskini. Bali kuwapa
jamaa ni bora kuliko kuwapa watu wageni kwa sababu kuwapa jamaa ni sadaka na
pia kuunga ukoo. Lakini sharti kwamba kuwapa sio kwa kuhifadhi mali yake mtu,
yaani ikiwa huyo jamaa masikini ni ambaye anapasa kumhudumia. Katika hali hii,
hairuhisiwi kumtimizia haja zake kwa kumpa Zakaah kwa sababu akifanya hivyo
atakuwa amehifadhi pesa zake mwenyewe kwa kumpa yeye Zakaah na hivyo
hairuhusiwi. Lakini ikiwa hana mas-uliya naye ya kumhudumia basi anaweza kumpa
Zakaah yake, na kumpa Zakaah yake ni bora kuliko kumpa mtu mgeni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Sadaka yenu kwa jamaa ni sadaka na pia kuunga ukoo)) [mwisho wa
kunukuu]
Kwa hiyo, hairuhusiwi kwako kuitoa
Zakaatul-Fitwr yako kumpa mama yako, bali umhudumie kutokana na mali yako
nyingine isiyokuwa ya Zakaah. Na tunamuomba Allaah Akuruzuku rizki kwa
wingi"
Na Allaah Anajua zaidi
MtotoWa Kiume Ana Uwezo
Mzuri Wa Kifedha Lakini Baba Yake Anashikilia Kumtolea Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Baadhi ya Baba wanashikilia
kuwatolea Zakaatul-Fitwr watoto wao wakiume ambao wana uwezo mzuri wa kifedha.
Afanyeje mtoto?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Madamu mtoto anao uwezo, inampasa
atoe mwenyewe Zakaatul-Fitwr. Ikiwa Baba atamlipia Zakaatul-Fitwr hakuna ubaya
khaswa ikiwa ni mazoea ya Baba kuwatolea watoto wake Zakaatul-Fitwr kila mwaka
japokuwa wameshakuwa wakubwa na wafanyakazi. Huenda akapenda kuendelea kufanya
hivyo alivyozoea kabla na huenda ikamkasirisha Baba ikiwa mwanawe atamwambia:
"Usinilipie Zakaah". Hivyo mtoto ampe fursa Baba yake kumlipia
Zakaatul-Fitwr na pia mwenyewe ajitolee. Baadhi ya watu wanachukulia kwamba
kuendelea kuwatolea watoto wao Zakaah ni kuendeleza kuambatana na watoto wake
na dalili ya kwamba wao bado wako chini ya hifadhi na mas-uliya yake. Hivyo
mtoto ampe Baba yake fursa afanye kinachomfurahisha.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Atujaalie tutekeleze yanayopasa kwetu.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid
Zakaatul-Fitwr Ni
Chakula, Sio Pesa Na Itolewe Kwa Waislamu Wanaohitaji Pekee
SWALI:
Kitu gani unatoa kwa ajili ya
Zakaatul-Fitwr? Ni pesa au mbegu? (chakula). Vipi ikiwa humjui mtu wa kumpa?
Je, inaruhusiwa kuitoa katika miskitii au kwa kafiri asiye na mahali pa kuishi
au kafiri kwa ujumla?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Ibn 'Umar (Radhiya
Allaahu 'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) aliifanya kutoa saa' ya tende au saa' ya shayiri (ngano) kuwa ni
Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na
mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda
kuswali (Swalaatul-'Iyd) [Al-Bukhaariy 1503]
Abu Sa'iydil-Khudriyyi
(Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr saa'
moja ya chakula, au saa' ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao
zama hizo) au saa' ya tende au saa' ya aqit (mtindi mkavu) au saa' ya
zabibu" [Al-Bukhaariy]
Kwa dalili hizo, ni dhahiri kwamba
Zakaatul-Fitwr lazima iwe ni chakula, sio pesa. Hivyo lazima tutekeleze
ilivyoamrishwa katika Sunnah. Hivyo lipa saa' moja ya chakula chochote
kinachotumika na watu katika nchi yako mfano mchele au ngano kwa ajili yako na
kila mtu katika nyumba yako. (saa' ni sawa na taqriban Kilo 3). Hairuhusiwi
kumpa yeyote isipokuwa Muislamu mwenye kuhitaji. Ikiwa hutopata mtu wa kumpa
katika nchi yako, unaweza kumwakilisha mtu mwingine akulipie katika nchi
nyingine.
Tunamuomba Allaah Atusaidie pamoja
na wewe kutimiza yapasayo Anayoyapenda.
Na Allaah Anajua zaidi.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid
Kuwakilisha Katika Kulipa
Zakaatul-Fitwr (Sadaka Ya Mwisho wa Ramadhaan)
SWALI:
Baadhi ya miskiti wanaashiria
kupokea kiwango cha Zakaatul-Fitwr kutoka kwa watu ili wagawe kwa wanaohitaji
kwa ajili yao. Hugawa bidhaa kama mchele, unga n.k. Je, desturi hii ni
sawa?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Kwa vile imekusudiwa kununua na
kugawa bidhaa kwa wanaohitaji (hizo bidhaa) kwa ajili yao, hivya ni sawa
na watapa thawabu Insha Allaah.
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid
Wapi Itolewe
Zakaatul-Fitwr?
SWALI:
Mimi ni kijana ninayeishi Zanzibar,
lakini nimepeleka mtoto wangu wa kike Uingereza kwa ajili ya matibabu na
nimefunga Ramadhaan Uingereza. Inanipasa nilipe Zakaatul-Fitwr Uingereza au
niwakilishe familia yangu Zanzibar kunilipia? Nini hukmu ya kulipa
Zakaatul-Fitwr kwa pesa? Tafadhali tanbihi kwamba Uingereza watu hutoa pesa
badala ya chakula.
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Maulamaa (Allaah Awe Radhi Nao)
wamesema kwamba Zakaatul-Fitwr inaambatana na idadi ya watu, sio pesa hivyo
ilipwe mahali ambapo mtu atakuweko usiku kabla ya 'Iyd.
Ibn Qudaamah amenukuu katika
Al-Mughniy [4/134]
"Ama Zakaatul-Fitwr ilipwe
katika nchi ambayo yule apasaye kulipa yuko, ikiwa ni mali yake iko hapo au
haipo hapo" [mwisho wa kunukuu].
Ama kuhusu kulipa Zakaatul-Fitwr kwa
pesa, tumeelezea katika jibu la 'Kiwango Cha Zakatul-Fitwr' kwamba lazima
ilipwe katika mfumo wa chakula na kwamba kulipa pesa haikubaliwi.
Hivyo lazima ujitahidi kulipa kwa
mfumo wa chakula. Ikiwa masikini atakaata chakula na akataka pesa, basi hakuna
ubaya kumpa pesa katika hali hiyo kwa sababu ya kuhitajika zaidi.
Na
Allaah Anajua zaidi
Inafaa Kutoa
Zakaatul-Fitwr Kwa Familia Ya Mkewe Ambao Wanahitaji?
SWALI:
Inafaa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa
familia ya mke wangu ambao wanahitaji?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Zakaatul-Fitwr itolewe kwa masikini
na wanaohitaji kwa sababu Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu
'anhuma) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
alifaradhisha Zakaatul-Fitwr kuwapa masikini iwe kama ni kutwaharisha Swawm ya
mfungaji kutokana na maneno ya upuuzi na machafu" [Imesumiliwa na
Abu Daawuud [1609] na ikapewa daraja ya Hasan na An-Nawawiy katika al-Majmuu'
[6/126] na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abi Daawuud]
Ikiwa familia ya mke wako ni
masikini na wenye kuhitaji, hakuna ubaya kuwapa Zakaatul-Fitwr, bali ni bora
zaidi kuliko kuwapa wengine kwa sababu familia ya mke wako (wakwe, mashemeji,
mawifi) wana haki kuwahudumia kama ni sehemu ya kumheshimu mke na kumtendea
wema na upole.
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Allaah
Amrehemu) amesema katika an-Nuur 'alaa ad-Darb [682]:
"Hakuna shaka kwamba wakwe,
mashemeji na mawifi wana haki ambazo ni zaidi ya mtu mwengine yeyote"
[mwisho wa kunukuu]
Tunamuomba Allaah Akujaalie thawabu
za sadaka na thawabu za kuwahudumia na
kuwatendea wema familia ya mke wako kwa huruma"
Na Allaah Anajua zaidi
Shaykh Muhammad Swaalih Al-Munajjid
Zakaatul-Fitwr Igaiwe Kwa
Mtu Mmoja Au Watu Mbali Mbali?
SWALI:
Je, Zakaatul-Fitwr ni kwa ajili ya
mtu mmoja pekee au igaiwe kwa wengi?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr kwa
mtu mmoja kwa ajili ya mtu mmoja na inaruhusiwa pia kuigawa kwa
watu zaidi ya mmoja.
Na Allaah ni Mweza wa yote..
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa
Kiislaam na utoaji wa Fatwa. Fatwa Namba 1204
Zakaatul-Fitwr Ni Fardhi
Kwa Masikini Pamoja Na Familia Yake?
SWALI:
Mtu masikini mwenye majukumu ya
familia yake ambayo ni miongoni mwa mama, baba na watoto. 'Iydul-Fitwr inawadia
naye ana saa' tu ya chakula. Amlipie nani?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Ikiwa hali ya masikini huyu ni kama
ilivyoelezewa katika Swali, hivyo alipe saa' ya chakula kwa ajili yake kwani ni
ziada ya mahitajio yake na mahitajio ya wale ambao ni wajibu wake kuwahudumia
mchana na usiku wa 'Iyd, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) kasema: ((Anza kwa nafsi yako kisha kwa
wanaokutegemea)) [Imesumulia na Al-Bukhaariy 2/117, 6/190, Muslimi
2.717, 718, 721, 1034, 1036, 1042]
Kuhusu wanaomtegemea ikiwa hawana
chochote cha kujitolea katika Zakaah kwa nafsi zao wenyewe, basi hawakuwajibika
kulipa kwa sababu Allaah Anasema:
((Allaah
Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo))
[2: 286]
Na Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna sadaka isipokuwa
kwa yule mwenye njia [mwenye uwezo])) [imesimuliwa na Al-Bukhaariy
2/117, 6/190, Muslim 2/717 Namba 1034. Naye (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ninapokuamrisheni kufanya
jambo, basi fanyeni kadiri muwezavyo)).
Na Allaah ni Mweza wa yote..
Tunamuomba Allaah Amrehemu Mtume Muhammad na Ahli yake na Maswahaba.
Halmashauri ya Kudumu ya Utafiti Wa
Kiislaam na utoaji wa Fatwa
Kuwalipia Makafiri
Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Watu wengi wana wafanyakazi wa
nyumbani (housemaids) wasio Waislamu. Je, walipiwe Zakaatul-Fitwr au inafaa
kuwapa chochote katika Zakaatul-Fitwr?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Hawalipiwi Zakaatul-Fitwr na haipasi
wao kupewa Zakaatul-Fitwr. Ikiwa mtu atawapa baadhi ya Zakaah, haitoshi (kwa
maana atakuwa hakutimiza wajibu wa kuilipia). Lakini anaweza kuwatendea wema na
kuwapa chochote ambacho hakitokani na Zakaah inayowajibika (kama Zakaatul-Fitwr
au Zakaah ya mali inayotimia mwaka).
Na Allaah Anjua zaidi
Wanaishi Nchi Za
Ki-Magharibi Na Hawaoni Masikini Wa Kuwapa, Wanaweza Kutuma Zakaatul-Fitwr Nchi
Nyingine?
SWALI:
Sisi ni wa-Tanzania tunaoishi
Uingereza na hatujui watu masikini wowote hapa. Tumepata mtu wa kuaminika
Insha-Allaah, ambaye amesema: "Nipeni pesa nitanunua mchele nusu yake na
kugawa kwa masikini, na nusu yake nitawapa pesa". Sababu yake ni kwamba
tuko zaidi ya watu 500 hivyo itakuwa shida kwake kununua kiasi kikubwa cha
chakula na kukibeba. Pia kwa vile masikini pengine wasitake chochote ila pesa
kwa sababu wataweza kuzitumia vizuri zaidi kuliko kupata mchele. Je tumpe pesa
au tuwakilishe ndugu zetu huko Tanzania ili watutolee?
JIBU:
Sifa Zote Ni Za Allaah
Rai ya Maulamaa wengi (wakijumuuisha
Maalik, ash-Shaafi'y na Ahmad) ni kwamba hairuhusiwi kutoa pesa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr,
bali lazima itolewe kama chakula kama ilivyoamrisha na Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) [Al-Bukhaariy (1504) na Muslim (984) iliyosimuliwa
na Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba: "Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr saa'
moja ya tende au saa' moja ya shayiri (ngano) kwa kila mtu, aliye huru au
mtumwa, mwanamume au mwanamke, miongoni mwa Waislamu"
Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu
Allaah) aliulizwa:
"Masikini wengi siku hizi wanasema kuwa
wanapendekezea kupokea Zakaatul-Fitwr katika mfumo wa pesa badala ya chakula
kwa sababu zina manufaa zaidi kwao. Je, inaruhusiwa kutoa pesa kwa ajili ya
Zakaatul-Fitwr?
Kwa msaada
wa: www.alhidaaya.com
No comments:
Post a Comment