THE
UNITED REPULIC OF TANZANIA
MINISTRY
OF LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT
Telegrams: Scientific Mtwara
Tanzania Livestock Research Institute
Tel: +255 073 293 4035 Naliendele
Fax: +255 073 293 41
P. O.
Box 509
Email: utafiti@iwayafrica.com MTWARA
In
reply please quote:
Kumb
Na. MLD/NAL/F/2/Vol. 1/38
KWA YEYOTE ANYEHUSIKA:
YAH:
NAFASI ZA KAZI KATIKA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO (TALIRI) NALIENDELE-MTWARA
Tafadhali rejeeni kichwa cha
habari hapo juu.
Napenda kuwatangazia
kuwa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) iliyoanzishwa kwa Sheria
Namba 4. Ya mwaka 2012 ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo nafasi
za kazi kwa wale watakaopenda kufanya kazi katika Taasisi ua Utafiti wa Mifugo
Naliendele-Mtwara. Nafasi zilizopo kwa sasa ni kama ifuatavyo:
(1)
Katibu muhtasi nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na Certificate au Diploma
ya Secretarial duties kutoka chuo kinachotambulika (2) Awe na uzoefu wa miaka
angalau mitatu kazini (3) Awe na typing speed ya 50 w.p.m (4) Awe na short hand
80 w.p.m (5) Awe anafahamu kutumia Computer.
(2)
Afisa Ugavi nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na Diploma in Supplies
and Procurement au Business Administration au Materials Management (2) Awe na uzoefu
usiopungua miaka mitatu (3) Awe anafahamu kutumia Computer.
(3)
Mhasibu nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na ATEC I au ATEC II au
Diploma ya uhasibu (2) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu kazini (3) Awe
anafahamu kutumia Computer.
(4)
Masjala nafasi (2)
Sifa: (1) Awe na Diploma ya Records Management au Archive Administration kutoka vyuo
vinavyotambulika (2) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu kazini (3) Awe
anafahamu kutumia Computer.
(5)
Mapokezi nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na cheti cha Elimu
ya Sekondari (ACSE) ambacho amefaulu somo la Kiingereza na
Kiswahili (2) Awe amewahi kufanya kazi ya namna hiyo kwa muda usiopungua miaka mitatu
(3) Awe na uwezo wa kuongea na kuandika Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
(6)
Walinzi nafasi (2):
Sifa: (1) Awe amemaliza elimu ya msingi
au zaidi ya elimu ya msingi (2) Awe amemaliza mafunzo ya Mgambo au Jeshi la
kujenga Taifa (JKT) (2) Awe na uzoefu wa kazi ya ulinzi katika taasisi yoyote
inayotambulika usiopungua miaka mitatu (3) Awe hodari na mwaminifu.
Namna
ya kutuma maombi:
Tuma
barua iliyosainiwa na mwajiri wako na ambatanisha CV na vivuli vya vyeti na
nyaraka nyingine muhimu kwenda kwa: Kaimu Mkurugenzi, Taasisi ya Utafiti
wa Mifugo Tanzania (TALIRI), S. L. P 202, Mpwapwa-Dodoma.
Imetolewa na:
Dr. Ezekiel H.
Goromela
MKURUGENZI-TALIRI
NALIENDELE
No comments:
Post a Comment