Kuna umuhimu mkubwa wa kuzungumzia kuhusu roho (nafsi) zetu ambazo zinahitaji
kutoharishwa ili ziwe katika hali ya asili yake, (kama
zilivyokuwa kabla ya kupulizwa katika mwili wa binaadamu) na ambazo
ndio zitakuwa sababu ya kufaulu au kufeli kwetu duniani na
akhera.
((وَيَسْأَلُونَكَ
عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّن الْعِلْمِ
إِلاَّ قَلِيلاً))
((Na wanakuuliza (ewe Muhammad) khabari
za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika
ilimu ila kidogo tu)) [Al-Israa::85]
Roho
ni siri Yake kubwa Allaah سبحانه وتعالى kwani
hata mtu awe mtaalamu au hodari wa hali ya juu kabisa,
lakini hatoweza kuumba hata chembe ya kidudu. Allaah سبحانه وتعالى Ametoa changamoto kubwa
sana kwa wale wote ambao wanaabudu miungu isiyokuwa Allaah سبحانه وتعالى kwa kuwapa mfano mdogo wa aina
yake! Kuwataka kuwaonyesha kuwa hao miungu wanaowaabudu si lolote si chochote
na hawawezi kuwasaidia wao wenye kuwaabudu bali hata kujisaidia wenyewe!! Na
matokeo yake ni udhalili wa kudumu.
((يَا
أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ
اللَّهِ لَن يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ وَإِن يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَّا
يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ))
((Enyi watu! Unapigwa mfano,
basi usikilizeni. Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah, hawatoumba hata nzi
ijapo kuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata
kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa)) [Al-Hajj:
73]
Allaah سبحانه وتعالى alikusanya kizazi chote cha Adam عليه السلام (kabla ya kuwaumba duniani) na
wakati huo roho zao zilikuwa ni safi kabisa zilizo katika
"Fitrah" (maumbile ya asili ya Uislam). Nasi (viumbe)
tukashuhudia na kuchukua ahadi kwamba tutamtii Mola wetu.
((وَإِذْ
أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى
أَنفُسِهِمْ أَلَسْتَ بِرَبِّكُمْ قَالُواْ بَلَى شَهِدْنَا أَن تَقُولُواْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ
إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ))
((Na pale Mola wako Mlezi Alipowaleta
katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya
nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Ndiye!
Tumeshuhudia (kuwa Wewe ndiye Mola wetu) (Allaah Akawaambie). Msije mkasema
Siku ya Qiyaamah sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo)) [Al-A'araaf :172]
Hali hiyo ya
'Fitwrah' ina maana kwamba, Allaah سبحانه وتعالى Katuumba katika hali ya
kuikubali dini Yake na kutupa Imani ya kuamini Tawhiyd, (kuwa Yeye ni
Mungu Mmoja pekee hana mshirika) Aayah hii ifuatayo, Anatuamrisha tuelekee
katika hii dini tukufu ya Kiislamu iliyo na muongozo kamili kwa viumbe wote.
((فأقم
وجهك للدين حنيفا فطرة الله التي فطر الناس عليها لا تبديل لخلق الله))
((Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini -
ndilo umbile la Allaah Alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa
Allaah. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui)) [Ar-Ruum:30]
Mtume صلى الله عليه وسلم ametuthibitishia haya kwa kubainisha kuwa ni wazazi wa mtoto ndiyo
wanaobadilisha Fitrah hiyo:
عن أبا هريرة رضي الله عنه
كان يحدث : قال النبي صلى الله عليه وسلم : ((ما من مولود إلا يولد على الفطرة، فأبواه يهودانه أو ينصرانه أو يمجسانه، كما تنتج البهيمة
بهيمة جمعاء، هل تحسون فيها من جدعاء)). ثم يقول أبو هريرة رضي الله عنه : ((فطرة الله التي فطر الناس عليها)) أخرجه
البخاري و مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrha رضي الله عنه ambaye alisema :
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema;
((Kila kizazi (mtoto mchanga) anazaliwa katika 'Fitwrah' kisha wazazi wake
humbadilisha na kumuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unasara au Umajusi, kama
mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe
kama yeye, je, mtaona (mtahisi) kuwa hana pembe (na hali anayo)?)) Kisha Abu
Hurayrah akasoma Aayah isemayo: ((Ndilo umbile la Allaah Alilowaumbia
watu)) [imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Baada ya
kutuumba Allaah سبحانه
وتعالى
kwa Rahma Yake Akatutumia uongofu
(ambao ni Mitume Yake na vitabu Vyake) uwe unatukumbusha kila mara
tuimarishe Imani zetu na kutuongoza katika njia
iliyo nyooka sawasawa.
))فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم
مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلا يَشْقَى((
((Na ukikufikieni Uongofu kutoka Kwangu basi
atakayeufuata uongofu Wangu, hatapotea wala hatataabika)) [Twaahaa:122]
Kufuata uongofu
huo vile vile ni kama mtihani kwetu Apate kupambanua Allaah سبحانه وتعالى nani katika sisi atakuwa
bora Kwake.
((الَّذِي
خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا))
((Ambaye Ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni
nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi)) [Al-Mulk:2]
Lakini ni hiari
ya mtu kuufuata huo uongofu au kuupuuza na kupotea katika njia mbaya.
((هَلْ أَتَى عَلَى
الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا)) (( إِنَّا خَلَقْنَا
الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا
بَصِيرًا)) ((إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورً))
((Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama
ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa)) ((Hakika Sisi Tumemuumba mtu
kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, Tumfanyie mtihani. Kwa hivyo
Tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona)) ((Hakika Sisi Tumembainishia njia.
Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru)) [Al-Insaan: 1 –
3]
Baada ya
kutuumba kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, yaani mwanamke anaposhika
mimba na inapofika miezi minne Allaah سبحانه وتعالى humtuma Malaika wake kupuliza
roho ya huyo kiumbe akawa sasa ni binaadamu, na Malaika huyo huamrishwa
kumuandikia mambo manne:
عن أبي عبد الرحمن عبد الله بن مسعود -رضي الله عنه- قال حدثنا رسول
الله -صلى الله عليه وسلم- وهو الصادق المصدوق: ((إن أحدكم
يُجمع خلقه في بطن أمه أربعين يوماً نطفة، ثم يكون علقة مثل ذلك، ثم يكون مضغة مثل ذلك، ثم يرسل إليه
الملك فينفخ فيه الروح، ويؤمر بأربع كلمات: بكتْبِ رزقه، وأجله، وعمله، وشقي أو سعيد، فوالله الذي لا إله
إلا غيره إن أحدكم ليعمل بعمل أهل الجنة حتى ما يكون بينه وبينها إلا ذراع فيسبق عليه الكتاب فيعمل بعمل أهل
النار فيدخلها، وإن أحدكم ليعمل بعمل أهل النار حتى ما يكون بينه وبينها إلا ذراع فيسبق عليه الكتاب فيعمل
بعمل أهل الجنة فيدخله))ا رواه
البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abu 'Abdur-Rahmaan 'Abdullaah bin Mas'uud (Radhiya
Allaahu 'anhu) kwamba: "Ametuelezeza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa ((Hakika kila mmoja
hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni
mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa
ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah
Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno
manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake,
mtu muovu au mwema. WaLlaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye,
hakika mmoja wenu huenda afanye vitendo vya watu wa Peponi hadi ikawa baina
yake na pepo ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya amali
ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya vitendo vya watu wa
motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa
kikathibiti akafanya amali ya watu wa peponi akaingia peponi.)) [Al-Bukhaariy
na Muslim]
Hapa tena
itakuwa ni vitu viwili vimekusanyika, nafsi na mwili na ndio maana mtu
anapokufa tunasema 'fulani amefariki'. Neno la kufariki ina maana
kutengana, yaani roho imetengana na mwili na kila kitu kinarudi kule kwenye
asili yake. Roho inarudi juu kwa Muumba wake na mwili unarudi ardhini
kwenye udongo ambapo ndio chanzo cha kuumbwa kwake.
KWA MSAADA WA www.alhidaaya.com
No comments:
Post a Comment