Matokeo ya Darasa la Saba yametangazwa jana na mwaka huu ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka
jana mbaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya
mtihani mwaka huu wa darasa la saba kufaulu zaidi ukilinganisha na
wanafunzi wa mwaka jana.
Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles
Msonda amesema ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya
6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012 Mwaka huu watahiniwa wamefaulu
zaidi katika somo la Kiswahili kwa asilimia 69.06 na somo walio
faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa
asilimia 28.62, Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya
844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya
250 idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61.