MAGAZETINI LEO JUMANNE TAR 12/02/2013: HANDAKI NDEFU BAHARINI, PAPA BEENEDICT XVI AJIUZULU.
Tuesday, February 12, 2013
Monday, February 11, 2013
VURUGU ZA KIDINI GEITA
Majeruhi Sadick Yahya
Polisi na raiya
majeruh Said Ntahompagaze aliyejeruiwa mguu
Polisi na raiya
Imeripotiwa katika mitandao mbali mbali kuwa leo zimetokea vurugu
za kidini nchini kati ya Waislam na Wakristu, katika kijiji cha
Buselesele Wilayani Chato Mkoani Geita na kupelekea
watu 10 kujeruhiwa vibaya huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste
Assemblies of God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha chanzo cha vurugu hizo kikiwa ni mvutano katika uchinjaji wa
wanyama kwa ajili ya kitoweo.
Mbali na mchungaji huyo kupoteza maisha, wengine
waliojeruhiwa ni pamoja na Said Ntahompagaze(45), Sadick Yahaya(40), Yasin
Rajab(56), Vicent Damon(22), wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika
hospital ya wilaya ya Geita.
Kwa sasa Waislam ndio wanaotambulika kuwa na dhamana ya kuchinja
katika mchinjio ya serikali.
Friday, February 8, 2013
ALLAH HATAZAMI MIILI WALA SURA, BALI ANATAZAMA NYOYONI
Hadiyth Ya 1, Katika kitabu cha Hadithi za Mtume (s.a.w.): LU-ULU-UN MANTHUWRUN
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ
(رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله
وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسَامِكُمْ وَلاَ إِلَى
صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa
Abu Hurayrah (رضي
الله عنه) amesema: Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala
sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu)).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Umuhimu wa kuwa na niyyah safi na ikhlaasw katika kumuabudu Allaah (سبحانه وتعالى) kwani hivyo ndivyo tulivyoamrishwa:
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا
اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا
الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ
((Na hawakuamrishwa ila kumwabudu
Allaah kwa kumtakasia Dini, hunafaa [wakielemea Dini ya haki na kuacha Dini
potofu] na wasimamishe Swalaah, na watoe Zakaah, na hiyo ndiyo Dini iliyo
sawa)).[2]
- Hima ya kutenda ‘amali njema baada ya kuwa na niyyah safi.
- ‘Amali na ‘Ibaadah hazipokelewi isipokuwa niyyah ikiwa ni safi kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Kahf 18: 103-104, 110, Al-Furqaan 25: 23].
- Hakuna ajuaye yaliyo moyoni mwa mja isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) [Al-Mulk 67: 13, Huwd 11: 5, Faatwir 35: 38, Al-Hadiyd 57: 6, At-Taghaabun 64: 4].
يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا
تُخْفِي الصُّدُورُ
(([Allaah] Anajua hiyana ya
macho na yanayoficha vifua)).[3]
- Binaadamu hawezi kuficha kitu kwa Allaah, kwani ‘amali na siri zote zitadhihirika Siku ya Qiyaamah. [Aal-‘Imraan 3: 29, Az-Zumar 39: 7, Al-An’aam 6: 60, At-Tawbah: 94, Al-Jumu’ah 62: 8, Atw-Twaariq 86: 9].
- Ni muhimu kwa Muislamu kuzitekeleza amri za Dini yake na si kwa mandhari pekee. Na mara nyingi watu huwa ni wenye kusema pindi anapotenda jambo ovu kuwa: “Lakini niyyah yangu ni nzuri”. Hapa Muislamu anatakiwa aizingatie Hadiyth nyengine inayosema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo na ‘amali zenu)).[4] Hivyo, ‘amali zinafaa ziende sambamba na Aliyoyateremsha Allaah na kuja nayo Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
- Usimhukumu mtu kwa mandhari yake, pindi ukimuona mtu shakili yake na hakuvaa mavazi ya Muumin ukadhania ni mtu muovu, huenda akawa ni mwema. Hali kadhalika, pindi ukimuona mtu shakili yake na mavazi yake ni ya ki-Muumin ukadhani kuwa ni mtu mwema kabisa, lakini huenda akawa ni mtu muovu.
- Kuzingatia yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) daima.
1 Muslim
2 Al-Bayyinah (98:5)
3 Ghaafir
(40:19)
4 Muslim
Saturday, February 2, 2013
TAARIFA YA MKUTANO
Sheikh Ponda Issa Ponda na Swalehe Mukadam wenye kanzu kutoka kushoto
Waislam wote wa Dar es Salaam na maeneo jirani mutangaziwa kukutana kesho inshaallah Juma Pili tarehe 03-Feb-2013
Kwanzia Saa 4 Asubuhi-Mchana. katika Kiwanja cha Nuurul Yaqiin (Uwanja wa Pamba) karibu na Uwanja wa Mwembe Yanga. Wilaya ya Temeke
katika Mkoa wa Dar es Salaam, kujadili nini cha kufanya kuhusu mateso
dhidi ya Masheikh wanaoteseka rumande Shekhe Ponda Issa Ponda na Swalehe
Mukadam.
Hatua hiyo, inatokana na Masheikh hao kuendelea kusota
rumande baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuweka hati ya kuzuia
dhamana dhidi yao.
Sisi kama waislamu tunatakiwa kushikamana katika kamba moja kwa hali na mali, ndugu muislamu upatapo taarifa hii muarifu na mwingine kwani uwepo wako ndio mafanikio ya mkusanyiko huo. Hakuna atakaye tufanyia mambo yetu sisi waislam zaidi ya sisi wenyewe.
Shime alaykum, kujitokeza kwa wingi ili kuonesha mshikamano kaika jambo hili muhimu.
Mwisho
Taarifa hii ni kutokana na: https://www.facebook.com/groups/ahlusunatv/428525543893691/?notif_t=group_activity
Subscribe to:
Posts (Atom)












