Tuesday, July 30, 2013

MASIKU YA KUMI LA MWISHO LA MWEZI WA RAMADHAN


Masiku ya kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani, yana fadhila na khususia nyingi kathiri, miongoni mwake ni pamoja na kwamba:
i. Ndani ya masiku hayo umo usiku wa cheo/heshima, ambao huo ni bora kuliko miezi alfu moja. Na ye yote atakaye simama kufanya ibada katika usiku huo, kwa kumuamini Allah kikweli na kwa kutaraji ujira kutoka kwake, huyo atasamehewa dhambi alizokwisha zitenda.

Saturday, July 6, 2013

MWEZI WA RAMADHAAN IMETEREMSHWA QUR-AAN - JICHUMIE FADHILA ZA KUSOMA NA KUHIFADHI QUR-AAN

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  
(( شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))

((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 184]
Kwa hivyo basi ndugu Muislamu, jitahidi ufanye ibada hii adhimu usome na kuhifadhi Qur-aan kwa wingi kabisa kwani thawabu na fadhila zake ni nyingi na adhimu mno kama tunavyozinukuu humu. Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) japo mara moja Qur-aan nzima kabla ya mwezi wa Ramadhaan kwisha.