Monday, December 19, 2016

UMUHIMU WA KUCHUNGA WAKATI



Makala hii muhimu itagusia sana umuhimu wa Muislamu kuchunga muda wake na kutokuuangamiza kwa kufanya mambo ya kipuuzi ambayo hayatomsaidia si duniani wala Akhera. Waislamu wengi tunashinda siku kutwa na kujishughulisha na mambo ya kipuuzi ambayo mengi katika hayo hayamridhishi Allaah.
Kwanza kabla ya kuendelea tungelipenda kurudi nyuma kidogo tukumbushane lengo la sisi kuwa hapa duniani ni lipi, kwa nini MwenyeZimungu ametuumba. Allaah anasema katika Qur-aan:

”Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi”