Sunday, January 5, 2014

SIFA NNE ZA KUCHAGUA MKE MWEMA


Sifa Nne Za Kuchagua Mke: Mali, Nasaba, Uzuri Na Dini

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا, وَلِحَسَبِهَا, وَجَمَالِهَا, وَلِدِينِهَا. فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mwanamke huolewa kwa sababu nne; Kwa mali yake, nasaba yake [ukoo], uzuri wake na Dini yake. Tafuta mwenye Dini uwe salama)).[1]  (yaani usiharibikiwe katika maisha yako)

 Mafunzo Na Hidaaya:
  1. Uislamu umetoa uongofu katika kila jambo hata katika kutafuta mke mwema. 
  1. Kupata mke mwenye Dini ni sababu ya mume kupata utulivu katika maisha ya ndoa, kwani mke mwenye Dini atafuata shari’ah za Dini yake na atajitahadharisha kutokutoka nje ya mipaka. [An-Nisaa 4: 34]. Allaah Alionya hivyo kuhusu wake zake Mtume: 

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ وَأَبْكَارًا ﴿٥﴾ ثَيِّبَاتٍ
(Mtume) Akikutalikini, Mola wake Atambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Muslimaat (Waislamu), Muuminaat (Waumini), Qaanitaat (watiifu), Taaibaat (wanaotubia), ‘Aabidaat (wanaofanya ‘ibaadah), Saaihaat (wanaofunga Swawm au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah), Thayyibaat (wajane, waliowahi kuolewa), na Abkaar (bikra; hawajawahi kuolewa) [2]

  1. Mke mwenye Dini ni mwenye kumnufaisha mumewe katika kushirikiana kwa kila upande wa maisha yao, ikiwa ni wakati wa furaha na shida, malezi ya watoto, kuhifadhi mali yake, siri yake, nayo ni furaha kamili kwa familia yote [Hadiyth: ((Je, siwaambii hazina bora aliyonayo mwanamme? Ni mke mwema [mchaji Allaah]; ambapo anapomuangalia, anamfurahisha, na anapomuambia chochote, anamtii na anapokuwa hayupo nyumbani, anatizama [mke] maslahi ya mumewe)).[3]
  1. Mke mwenye Dini ni sababu mojawapo ya kuidumisha ndoa.
  1. Mke mwema mwenye taqwa ni sababu mojawapo ya kupata mafanikio ya duniani na Aakhirah. 
  1. Katika uchaguzi wa mume au mke, Dini inatakiwa ipatiwe kipaumbele. 
 
 
 Shukran: alhidaaya.com

No comments: