Sunday, November 3, 2013

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013, HAYA HAPA

 
 
Matokeo ya Darasa la Saba yametangazwa jana na mwaka huu ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mbaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba kufaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana.
Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012 Mwaka huu watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili kwa asilimia 69.06 na somo walio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62, Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61.
 

Saturday, November 2, 2013

Du’aa Ya Malaika Kila Siku Kwa Mtoaji Sadaka Na Mzuiaji

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ الْعِبَادُ فِيهِ إلاَّ مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُنْفِقًا خَلَفًا. وَيَقُولُ الأَخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا تَلَفًا)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah(رضي الله عنه)  kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila siku inayowapambaukia watu kuna Malaika wawili wanateremka, mmoja wao akiomba: Ee Allaah! Mwenye kutoa [sadaka] mlipe zaidi. Na mwengine huomba: Ee Allaah! Mwenye kuzuia mpe hasara)).[1]