Sunday, October 27, 2013

Mwanamke Asifunge Swawm Au Kumuingiza Mtu Kwenye Nyumba Bila Ya Idhini Ya Mumewe

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ يَحِلُّ لِلْمَرْأَةِ أَنْ تَصُومَ وَزَوْجُهَا شَاهِدٌ إلاَّ بِإِذْنِهِ. وَلاَ تَأْذَنَ فِي بَيْتِهِ إلاَّ بِإِذْنِهِ)) متفق عليه وهذا لفظ البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Si halali kwa mwanamke kufunga Swawm [ya Sunnah] ilhali mumewe yupo [hakusafiri] ila kwa idhini yake. Wala asimruhusu mtu kuingia nyumbani kwake ila kwa idhini yake)).[1]
 

Tuesday, October 22, 2013

Nimemdanganya Mume Wangu, Je, Nimeachika? Na Je, Inanipasa Nikae Eda


SWALI:
Bibi na Bwana wameelewana kutumia koil kukinga kupata mtoto kwa mda. Kisha bwana ameamua koil bibi akaitowe. Bibi akamwambia bwana haya. Ikapita mdaa. Bwana akamuuliza bibi kama ile koil ameitoa? Bibi akadaganya mumewe kwamba koil kesha itowa. Baadae siku kadha bwana akamwambia bibi nafikiri kua koil hujaitoa umenidaganya. Na kama umenidaganya jua nishakuwacha. Bibi ana watoto watatu. WA miaka mitatu, na miwili na mmoja. Kazi ya ulezi pekee yake. Sababu bwana anafanya kazi kuazia jumatatu hadi ijumaa.   Swala langu ni, jee huyu mwanake kishawachika? Swala la pili kwa kua anahakika kua anatumia koil kutokupata mimba jee. Jee akiachika anakaa edaa? Insha’Allah nitapata majibu ya kuniridhisha. Asalaam aleikum.