Wednesday, August 21, 2013

NAFASI ZA KAZI KATIKA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO (TALIRI) NALIENDELE - MTWARA


THE UNITED REPULIC OF TANZANIA
MINISTRY OF LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT

Telegrams: Scientific Mtwara                                   Tanzania Livestock Research Institute
Tel: +255 073 293 4035                                         Naliendele
Fax: +255 073 293 41                                            P. O. Box 509
Email: utafiti@iwayafrica.com                                  MTWARA
            In reply please quote:
            Kumb Na. MLD/NAL/F/2/Vol. 1/38

KWA YEYOTE ANYEHUSIKA:

YAH: NAFASI ZA KAZI KATIKA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO (TALIRI) NALIENDELE-MTWARA

Tafadhali rejeeni kichwa cha habari hapo juu.

Napenda kuwatangazia kuwa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) iliyoanzishwa kwa Sheria Namba 4. Ya mwaka 2012 ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazo nafasi za kazi kwa wale watakaopenda kufanya kazi katika Taasisi ua Utafiti wa Mifugo Naliendele-Mtwara. Nafasi zilizopo kwa sasa ni kama ifuatavyo:


(1)   Katibu muhtasi nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na Certificate au Diploma ya Secretarial duties kutoka chuo kinachotambulika (2) Awe na uzoefu wa miaka angalau mitatu kazini (3) Awe na typing speed ya 50 w.p.m (4) Awe na short hand 80 w.p.m (5) Awe anafahamu kutumia Computer.

(2)   Afisa Ugavi nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na Diploma in Supplies and Procurement  au Business  Administration  au  Materials Management (2) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) Awe anafahamu kutumia Computer.

(3)   Mhasibu nafasi (1)
Sifa: (1) Awe na ATEC I au ATEC II au Diploma ya uhasibu (2) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu kazini (3) Awe anafahamu kutumia Computer.

(4)   Masjala nafasi (2)
Sifa: (1) Awe na Diploma  ya  Records  Management  au  Archive Administration kutoka vyuo vinavyotambulika (2) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu kazini (3) Awe anafahamu kutumia Computer.

(5)   Mapokezi nafasi (1)
Sifa: (1)  Awe  na  cheti  cha  Elimu  ya  Sekondari  (ACSE) ambacho amefaulu somo la Kiingereza na Kiswahili (2) Awe amewahi kufanya kazi ya namna hiyo kwa muda usiopungua miaka mitatu (3) Awe na uwezo wa kuongea na kuandika Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.

(6)   Walinzi nafasi (2):
Sifa: (1) Awe amemaliza elimu ya msingi au zaidi ya elimu ya msingi (2) Awe amemaliza mafunzo ya Mgambo au Jeshi la kujenga Taifa (JKT) (2) Awe na uzoefu wa kazi ya ulinzi katika taasisi yoyote inayotambulika usiopungua miaka mitatu (3) Awe hodari na mwaminifu.

Namna ya kutuma maombi:
Tuma barua iliyosainiwa na mwajiri wako na ambatanisha CV na vivuli vya vyeti na nyaraka nyingine muhimu kwenda kwa:  Kaimu Mkurugenzi, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), S. L. P 202, Mpwapwa-Dodoma.

Imetolewa na:
Dr. Ezekiel H. Goromela
MKURUGENZI-TALIRI NALIENDELE

No comments: